Sudan Kusini yakumbwa na mlipuko wa Surua

0
24

Wizara ya Afya ya Sudan Kusini imethibitisha kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa surua katika mikoa/majimbo matano nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa Huduna za Magonjwa yanayozuilika, John Rumunu amethibitisha kuwepo kwa mlipuko huo lakini amesema bado hawana idadi kamili ya watu wangapi wameathirika, wangapi wamefariki na kuwatambua waliofariki.

Rumunu ameeleza kuwa wizara ya afya kwa kushirikiana na wadau wengine watatoa chanjo katika maeneo ambayo mlipuko huo umeripotiwa.

Shirika moja lisilo la serikali, Médecins Sans Frontiers (MSF) juma lililopita lilisema kuwa watoto 30 wanaougua surua walikuwa wakitibiwa katika kituo chao kilichopo eneo la Pibor, Mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika hilo limehimiza chanjo hiyo kutolewa kwa haraka ili kudhibiti kasi ya maambukizi mapya.

Send this to a friend