Tanzania yakanusha kuwekewa zuio na Umoja wa Ulaya

0
22

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ambaye pia ni Muwakilisha wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya (EU), Jestas Nyamanga amekanusha taarifa kuwa EU imeazimia kuinyima Tanzania mikopo na misaada.

Katika taarifa yake ya Novemba 19, 2020, Nyamanga amesema uamuzi huo haukutolewa na Bunge la EU bali ni hoja za wabunge watano wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge hilo.

Ameongeza kuwa kamati hiyo ina wabunge 70, na bunge zima lina wabunge zaidi ya 600, hivyo kusema hoja ziliotolewa na watu watano kuwa ni azimio la EU ni upotoshaji mkubwa.

Amesisitiza kuwa Tanzania na EU zina uhusiano mzuri tangu mwaka 1975.

Aidha, amewataka Watanzania kutokuwa na hofu na kuendelea na biashara zao na kupuuza uvumi kuwa Tanzania imezuiwa kuuza bidhaa zake kwenye nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Msikilize hapa chini akitoa ufafanuzi kwa kina;

Send this to a friend