Serikali yatangaza ajira elfu 13 za ualimu

0
29

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza ajira 13,000 za ualimu katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Magufuli alilolitoa Septemba 7 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Josepha Nyamhanga ametoa taarifa hiyo leo jijini Dodoma na kueleza kuwa 60% ya ajira hizo ni za walimu wa shule za msingi na 40% ni za walimu wa sekondari.

Walimu waliopata nafasi hizo wametakiwa kuanza kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia Disemba 1 hadi Disemba 14 mwaka huu.

Wakurugenzi wa halmashauri wametakiwa kuwasijili walimu watakaoripoti kwenye vituo vya kazi kwenye mfumo wa kanzi data ili wizara ijue waliowasili kwenye vituo vya kazi na waweze kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa ajira.

Send this to a friend