Serikali kuwahakiki wastaafu wote wanaolipwa na hazina

0
23

Wizara ya Fedha na Mipango inatarajia kufanya uhakiki wa wastaafu wanaolipwa pensheni na hazina kwa lengo la kuhuisha taarifa zao.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha imeeleza kuwa zoezi hilo litaanza Disemba 7, 2020 hadi Machi 7, 2021.

Wastaafu watahakikiwa kupitia kwenye halmashauri zilizoko kwenye wilaya zao wanapoishi.

Wahakikiwa watatakiwa kufika na barua ya tunzo la kustaafu au kitambulisho cha kustaafu, barua ya kustaafu au kustaafishwa, kitambulisho cha Taifa (NIDA) au kadi ya mpigakura

Aidha, watatakiwa kuwa na kadi ya bima ya afya, hati ya kusafiria au leseni ya udereva, na kadi ya benki wanapopokelea pensheni.

Wizara imesema kuwa zoezi hilo ni la lazima na kwamba wastaafu ambao hawatahakikiwa wataondolewa katika orodha ya malipo ya pensheni kuanzia Aprili 2021.

Send this to a friend