Waziri Mkuu atoa siku 7 walionunua magari kwa gharama kubwa wajieleze

0
30

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku saba kuanzia leo Disemba 17, 2020 kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, maofisa wanaochambua maombi ya ununuzi wa magari Ofisi ya Waziri Mkuu na wakurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Msalala na Kahama wajieleze kwa sababu gani magari kwa gharama kubwa.

Ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na watumishi wa umma, wabunge, madiwani katika jiji la Mwanza na Manispaa za Ilemela na Nyamagana na kusema kuwa magari hayo ni mzigo kwa wananchi.

Waziri Mkuu amesema hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma na haiwezekani viongozi hao watumie magari ya gharama kubwa badala ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na ametaka muongozo wa ununuzi wa magari, uliotolewa na serikali uzingatiwe.

Amesema matumizi ya fedha za umma lazima yasimamiwe ipasavyo na kwamba Serikali haina mzaha na mtumishi yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha za umma, hivyo amewataka madiwani wakasimamie vizuri maeneo yao.

Send this to a friend