Uganda: Polisi ammwagia pilipili machoni mgombea Urais wa upinzani

0
13

Mgombea wa urais nchini Uganda kupitia chama cha Forum for Democratic Change (FDC), Patrick Amuriat, amenyunyuziwa pilipili machoni kiasi cha kulazwa hospitalini.

Msafara wa Amuriat ulizuiwa na polisi alipokuwa safarini kwenda katika mkutano wa kampeni wilayani Tororo.

Amuriat, alifungua dirisha la gari lake kuzungumza na polisi kwenye barabara ya Bugiri kuelekea Tororo, na ndipo afisa wa polisi kwa jina Abraham Asiimwe alipomnyunyuzia pilipili machoni.

Tume ya uchaguzi imepiga marufuku kampeni katika wilaya ya Tororo, ambayo wachambuzi wa siasa Uganda wanasema ni ngome ya mgombea huyo wa upinzani.

Tume hiyo inasema wilaya ya Tororo ina maambukizi mengi ya virusi vya Corona na kampeni haziweki kufanyika wilayani humo.

Nyumbani kwa Amuriat ni wilayani Tororo.

Send this to a friend