Askari akutwa amejinyonga kwenye nyumba aliyokuwa anaijenga

0
13

Askari wa jeshi la polisi aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani namba E 6472 Yusuph Said (52) amekutwa amejinyonga hadi kufariki dunia katika nyumba yake anayoijenga katika maeno ya Miembe Saba, Kata ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea Januari 18, 2021 majira ya saa 12 jioni.

ASKARI wa jeshi la   Polisi Mkoa wa Pwani   mwenye  namba   E 6472   Yusuph Said  (52) ambaye ni mkazi wa Wilayani Kibaha aliyejinyonga  katika  nyumba yake aliyokuwa anaijenga katika maeneo ya kata ya Kongowe hadi kupoteza maisha  akiwa katika picha ya pamoja na askari wenzake  enzi za uwahi wake .(PICHA NA MAKTABA)  

Kamanda Wankyo amesema Yusuph aliyekuwa anaishi Picha ya Ndege alikuwa akitumika katika Kituo C lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.

Nyigesa amebainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa maziko zikiendelea.

Msaidizi wa balozi kwenye eneo hilo Imelda Kitosi amesema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani.

“Mimi sasa baada ya kupigiwa simu niliingia hapa pamoja na baadhi ya watu waliokuwa karibu tulimkuta yuko kwenye chumba ambacho kilikua kinajengwa kama bafu au choo kamba kaifunga juu na chini kulikua na tofali ambalo baada ya kuhangaika sana mguu mmoja tulikuta kama umepiga goti na mwingine umeegemea tofali huku kamba ikiwa shingoni” amesema Imelda

Balozi huyo alieleza kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo ndipo walipiga simu Polisi kutoa taarifa na walifika na kuchukua mwili wa marehemu.

Send this to a friend