Mwijage aitaka serikali iijenge sekta binafsi ya Tanzania

0
25

Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage ameitaka serikali kuijenga sekta binafsi ya Tanzania ili itumike katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Mwijage ametoa raia hiyo wakati akichangia mapango wa tatu wa maendeleo wa Taifa kwa miaka mitano 2021/22- 2025-26, na mapango wa maendeleo wa mwaka mmoja bungeni jijini Dodoma.

“… sekta binafsi inapaswa ikue, haikui. Wasikudanganye popote duniani sekta binafsi hujengwa,” ameeleza Mwijage akibainisha kuwa ili serikali iweze kukusanya mapato zaidi, ni lazima sekta hiyo ikue ili watu wawe tayari kulipa kodi.

Amesema baadhi ya watu wanahofu kuwa watapoteza fedha katika mchakato wa kujenga sekta binafsi, lakini amewaasa kuwa, mtu asipochafuka hawezi kujifunza.

“Wape wapoteze pesa watoke. Kuna haja ya kujenga sekta binafsi ya Tanzania.”

Kuhusu sekta ya viwanda ameeleza kuwa kujenga uchumi wa viwanda ni zaidi ya kujenga viwanda na kuwa, lazima watu wawe na utamaduni wa kuanzia chini, kuanza kidogo kidogo hadi kufikia pakubwa.

“Marehemu rafiki yangu Shaa wa A to Z alianza na chereheni moja, wakati anakufa alikuwa na kiwanda cha A to Z, alikuwa mlipaji kodi mkubwa kwa serikali,” ameeleza Mwijage ambaye amewahi pia kuwa waziri wa viwanda.

Send this to a friend