Vodacom Tanzania yazindua kampeni ya Mtandao Supa

0
20

Dar es Salaam.  Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayoongoza Tanzania Vodacom Tanzania PLC leo imezindua kampeni yake ya Mtandao Supa, kampeni yenye lengo la kuongeza ufahamu kwa wateja kuhusu mtandao wake wenye ubora wa hali ya juu na manufaa makubwa yanayopatikana kwa wateja wake katika mtandao huu supa wa Vodacom. (Super Vodacom network)

Kampuni ya Vodacom Tanzania inaona furaha kuwa na mtandao wenye nguvu zaidi nchini Tanzania wenye kasi ya 4G ya kupakua isiyo na mshindani ambayo inafikia mpaka mbps 27 ambayo ni karibu mara mbili ya kasi ya mtandao wa mshindani wake anayemfuata. Kampuni ya Vodacom imefanikiwa kufikia asilimia 90% ya idadi ya watu na kufika katika maeneo ya mjini na vijijini kutoa huduma zake za sauti, data na huduma za kifedha.

Akizungumza jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Bw. Hisham Hendi amaesema kampuni ya Vodacom imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano katika miaka iliyopita kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mtandao katika maeneo ya mijini na vijijini nchini.

“Jitihada za kampuni ya Vodacom Tanzania kuhakikisha kwamba Tanzania nzima imeunganishwa na inadhihirishwa kupitia uwekezaji wetu na mikakati yetu ya upanuzi wa upatikanaji wa huduma. Kuna wastani wa vituo kumi vya sauti na data vinavyojengwa, kupanuliwa au kuboreshwa katika siku moja kwa lengo la kutoa huduma ya uhakika na ubora wa hali ya juu kwa wateja wetu. Huu ni ushahidi katika jitihada zetu za kuhakikisha kwamba tunatoa huduma bora kwa wateja wetu. Tumewekeza zaidi ya shilingi bilioni 171.4 kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mtandao wa 4G katika miji mikubwa na kuboresha kiwango cha ubora wa mtandao wetu katika jitihada za kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia technolojia.” Alisema bwana Hendi.

Bwana Hisham anawahimiza watu wengi zaidi wanufaike na huduma hii ya kiwango cha juu kilichoko katika ofa kwa madhumuni ya kuboresha maisha yao kupitia teknolojia katika maeneo ya elimu, huduma kwa njia ya mtandao, biashara na burudani.

“Tunaamini katika nguvu ya teknolojia katika kubadilisha maisha ya jamii na kuleta mabadiliko chanya kwa watu binafsi, taasisi, biashara na sekta kama vile elimu ya afya na huduma za serikali kupitia mtandao,” alihitimisha bwana Hisham.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Vodacom Bi Linda Riwa alisema ili kuwaruhusu wateja wao kupata nafasi ya kufurahia nguvu hii mpya, kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua bando maalum linaloitwa BongelaBandoambalo ni la sauti na data. Bando hili linapatikana kwa kujisajili kila siku..

“Wateja wa Vodacom wanajisajili kwenye bando hii kwa kupiga *149*01# kisha chagua Internet au Cheka kuweza kujiunga na bando la Bongelabando ambalo linatoa 1GB kwa Tsh 1000, na dakika 300 kwa Tsh 1000 kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku”. Amesema.

Mkuu wa Kitengo cha Mtandao, Bwana Nguvu Kamando alisema uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Vodacom umewezesha mtandao wenye kasi na kuaminika zaidi nchini.

“Kampuni ya Vodacom imewekeza katika teknolojia bora na ya kiwango cha juu ambayo inawapatia wateja wake mtandao wenye kasi usio na mshindani, uunganishwaji wa uhakika popote wanapokuwa.”Alisema Kamando.

Send this to a friend