Bashungwa ataka wasanii kuwa na bima za afya

0
15

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amehimiza wasanii nchini kuhakikisha wanamiliki bima za afya ambazo zitawasaidia wanapokuwa wagonjwa wakati wowote.

Bashungwa amesema hayo alipomtembelea msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kikumbi Mpango, maarufu King Kikii Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Mei 22, 2021.

“Wizara itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yako na kwa sababu daktari wako tuna mawasiliano ya karibu tutakuwa tunajua hali yako inavyoendelea kila siku,” amesisitiza Bashungwa.

Kwa upande wake King Kikii amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kumtembelea na kumfariji pia amemuomba waziri amfikishie salamu zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuliongoza Taifa.

Mzee King Kikii ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanamuziki na wasanii wengine kuwa na nidhamu katika kazi ili kuendelea kufanya sanaa kwa muda mrefu.

Send this to a friend