Rais aiagiza BoT kujiandaa na matumizi ya sarafu za kimtandao (cryptocurrency)

0
35

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Benki Kuu ya Tanzania kujiandaa na matumizi ya safaru za kimtandao (cryptocurrecy/blockchain), kwani huenda ikafika wakati mabadiliko yanayotokea kwingineko yakaingia Tanzania.

Rais ametoa agizo hilo mapema leo wakati akizindua jengo la Benki Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, na kueleza kuwa mabadiliko ya teknolojia na kukua kwa utandawazi kunazidi kuleta mabadiliko mengi, ikiwamo kwenye sekta ya fedha.

“Tumeshuhudia kuibuka kwa safaru mpya kwa njia ya kimtandao. Najua bado nchini ikiwemo Tanzania hazijakubali au kuanza kuzitumia safaru hizo. Hata hivyo, wito wangu kwa Benki Kuu ni vyema mkaanza kufanyia kazi maendeleo hayo. Yakija yakitukamata, yasitukamate hatuko tayari,” ameagiza Rais Samia

Amesema kutokana na utandawazi, na licha ya kuwa Tanzania haijaruhusu au kuanza kutumia safaru hizo, wananchi wake wanaweza wakaanza kutumia huko nje ya nchi, na watakaleta jambo hilo nchini, ni muhimu maandalizi yawe yameshafanyika.

Nchi mbalimbali duniani tayari zimeanza kutumia safaru za kimtandao ambazo ni pamoja na Canada, Japan, Marekani, Ufilipino, Ufaransa, Australia, Nigeria.

Send this to a friend