Masuala la ugaidi na Corona yatawala mkutano wa SADC

0
13

Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) leo wamekutana mjini Maputo nchini Msumbiji katika mkutano wa dharura ambao umeongozwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi.

Miongoni mwa hoja kubwa zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na nchi wanachama wa ukanda wa SADC kushirikiana katika kukabiliana na tatizo la ugaidi linaloikabili Msumbiji, kwani limekuwa likirudisha nyuma juhudi za maendeleo kwa nchi hiyo na nchi wanachama.

Aidha, masuala mengine yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa dharura ni maambukizi ya Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (UVIKO 19), uanzishwaji wa kituo cha majanga, masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, biashara na Uwekezaji katika ukanda wa Jumuiya hiyo ya SADC.

Rais Nyusi amezisisitiza nchi wanachama kuendelea kuunga mkono jitihada za Taasisi za Utafiti katika kufuatilia taarifa za kusambaa kwa UVIKO 19 na mawimbi mapya ya ugonjwa huo na kuendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia maambukizi mapya.

Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maenendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), umefanyika sambambana na maadhimisho ya miaka arobaini tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo, ikiwa na kauli mbiu “ Kuimarisha Amani na Usalama, Kuhamasisha Maendeleo na Ustahamilivu wa Changamoto Zinazoikabili Dunia”.

Rais Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Msumbiji na kurejea Jijini Dodoma nchini Tanzania.

Send this to a friend