Wasifu wa CDF Jenerali Mabeyo ndani ya JWTZ
Jenerali Venance Mabeyo ni Mkuu wa Majeshi wa nane kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tangu alipoteuliwa Februari 6, 2017 na aliyekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Alizaliwa Julai 1, 1956 wilayani Magu mkoani Mwanza na kupata elimu ya msingi katika shule ya Namibu mkoani Mara kuanzia 1965 hadi 1971.
Alianza elimu ya Sekondari katika Seminari ya Nyegezi kuanzia 1972 hadi 1975, kisha akaendelea na kidato cha tano na sita Mzumbe Sekondari kuanzia 1976 hadi 1977.
Jenerali Venance Mabeyo alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Januari 1, 1979 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1980 kuwa Luteni Usu.
Safari ya Jenerali Venance Mabeyo JWTZ
Julai 1980: Luteni Usu
Agosti 1981: Luteni
Januari 1987: Kapteni
Oktoba 1991: Meja
Juni 1998: Luteni Kanali
Mei 2006: Kanali
Septemba 2010: Brigedia Jenerali
Septemba 2014: Meja Jenerali
Juni 2016: Luteni Jenerali
Februari 2017: Jenerali
Jenerali Venance Mabeyo alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadhi ya nchi hizo ni Kenya, India, Canada na Marekani
Jenerali Venance Mabeyo katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwambata Jeshi nchini Rwanda, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi , Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.
Jenerali Venance Mabeyo ametunukiwa medali mbalimbali;
Miaka 20 ya JWTZ
Medali ya utumishi mrefu.
Medali ya miaka 40 ya JWTZ.
Medali ya utumishi uliotukuka.
Medali ya Comoro na Anjouan.
Medali ya miaka 50 ya uhuru
Medali ya miaka 50 ya Muungano
Miaka 50 ya JWTZ
Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara