Mbunge wa Konde, Sheha Mpemba Faki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amejiuzulu nafasi hiyo leo Agosti 2, 2021 kutokana na changamoto za kifamilia.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka imeeleza kuwa chama hicho kimepokea kwa masikitiko makubwa barua ya kujiuzulu kwa mbunge hiyo.
Faki amejiuzulu ikiwa ni siku 16 tu zimepita tanguli alipochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 18, 2021, akiwa bado hajaapishwa.
Uchaguzi huo ulioshirikisha vyama 12 ulifanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Khatib Said Haji, aliyefariki Mei mwaka huu.
CCM imewagaka wanachama wake kuwa watulivu wakati taratibu nyingine zikifuata.