Denmark yaeleza sababu ya kufunga ubalozi wake Tanzania

0
16

Serikali ya Denmark imesema kuwa uamuzi wa kufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024 umetokana na vipaumbele vyake vipya kwenye ushirikiano na maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye mkakati wake mpya uitwao ‘The World We Are.’

Waziri Ushirikianowa Maendeleo wa Denmark, Flemming Mortensen amesema hayo wakati akizungumza kwa njia ya mtandao Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula na kusema kuwa uamuzi huo haukuwa rahisi kufikia.

Ameeleza kuwa mkakati huo unaitaka nchi hiyo kufanya kazi kwa karibu zaidi  na nchi zenye machafuko, hususani katika ukanda wa Sahel,  pembe ya Afrika na nchi jirani za kanda hizo ambazo zina matatizo ya kisiasa.

Serikali ya Tanzania imesikitika kufuatia hatua hiyo ikizingatiwa imefanya jitihada kubwa  kufufua na kuimarisha diplomasia na mataifa mbalimbali, kuimarisha biashara na uwekezaji  pamoja na kuimarisha demokrasia na utawala wa kisheria.

Balozi  Mulamula amemwambia Mortensen kuwa anaamini serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye masuala ya kimaendeleo na kuunga mkono ajenda za Tanzania katika jumuiya za kimataifa na majukwaa mengine.

Send this to a friend