Kwanini Royal Tour imekuja Tanzania wakati sahihi

0
50

Kwa siku kadhaa sasa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekuwa akizunguka katika mikoa mbalimbali na timu ya watalaamu kuandaa makala (documentary) inayolenga kutangaza vivutio vya kitalii na fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini Tanzania.

Huu ni muda sahihi sana kwa Tanzania kupata fursa hiyo kwa sababu uchumi wa dunia umeathirika sana UVIKO-19, na wakati chanjo ikiendelea kutolewa, nchi zimeanza kufungua mipaka yake, kuruhusu uchumi kukua tena.

Uamuzi wa Tanzania kutofunga uchumi wake kumeisaidia sana lakini huwezi kusema kwamba athari za ugonjwa huo hazijaigusa, kwani Tanzania sio kisiwa, inategemea pia mataifa mengine.

Kutokana na ugonjwa huo, idadi ya watalii waliokuwa wakija nchini ilipungua sana. Hivyo, jitihada kubwa zinahitaji kuitangaza tena Tanzania ili watalii hao waweze kuja, na ndio sababu ya kusema Royal Tour imekuja wakati sahihi sana, na wakti ambapo inahitajika.

Kupitia makala hiyo, Tanzania itaweza kutangaza duniani vivutio na mandhari zake za kuvutia ambavyo si tu vitakuza utalii, bali pia kubadili mtazamo wa dunia kuhusu nchi hii.

Nchi mbalimbali duniani zimetumia Royal Tour kuimarisha nafasi zake kwenye jukwaa la kimataifa, ambapo Rwanda ni moja ya nchi hizo, na imenufaika sana.

Hadi sasa Rais Samia amerekodi vivutio na fursa mbalimbali zilizopo visiwani Zanzibar, Bagamoyo, Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Mara.

Send this to a friend