Mtoto wa Museveni: Mapinduzi wa kijeshi yatadhibitiwa haraka
Mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema italichukua jeshi la nchi hiyo chini ya saa 24 kusambaratisha wanajeshi waasi watakaotaka kufanya mapinduzi kama yaliyomng’oa Rais wa Guinea, Alpha Conde.
Luteni Jenerali, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Kamanda wa Kamandi ya Jeshi la Ardhini aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa wanajeshi waasi watawajibishwa ipasavyo.
Katika ujumbe huo ameunganisha na picha ya Kanali Mamady Doumbouya ambaye ndiye aliongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea.
Wiki iliyopita Rais Museveni alitaka viongozi wa mapinduzi ya Guinea kuondoka akifafanua kuwa mapinduzi hayo ni kuirudisha nchi nyuma. “Tulikuwa nayo kwenye miaka ya 1960, yalikuwa sehemu ya mataizo ya Afrika, hivyo nalaani mapinduzi,” aliiambia French 24.
Rais wa Guinea alipinduliwa kwa kile jeshi ilichoeleza kwamba ni uongozi mbaya uliosababisha rushwa na umasikini kukithiri miongoni mwa wananchi.