Utaratibu unaotumika kukokotoa deni la Bodi ya Mikopo (HESLB)

0
48

Kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) wastani wa wanufaka 240 humaliza kulipa madeni yao kila mwezi. Bodi hiyo imekuwa ikiwahimiza wanufaika kulipa kwa wakati ili kuepuka tozo ya adhabu (penalty 0 ya 10%) ambayo huanza kutozwa baada ya miezi 24 tangu mnufaika ahitimu masomo.

Je! Unajua uataratibu unaotumika kufahamu malipo ya mnufaika. HESLB inakuchukua hatua kwa hatua kukujuza hilo;

Utaratibu wa Kikokotoo kwa mnufaika mwenye adhabu;

  1. Mnufaika aliyeajiriwa anapaswa kukatwa 15% tu ya mshahara wake

2. Ikiwa mshahara wake ni TZS 1,000,000.00 na amechelewa kuanza kurejesha atakatwa TZS 150,000.00 (15%) tu

3. Makato ya TZS 150,000.00 yatagawanywa kama ifuatavyo:
(a) TZS 1,500.00 ambayo ni Tozo ya 1% ya Uendeshaji (Loan Administration Fee – LAF)
(b) TZS 9,000.00 ambayo ni Tozo ya 6% ya kutunza thamani ya fedha za mkopo uliopewa ukiwa masomoni (Hata hivyo Rais Samia Suluhu Hassa alielekeza HESLB kuondoa tozo hii)
(c)TZS 15,000.00 ambayo ni adhabu kwa kuchelewa kuanza kurejesha ndani ya miezi 24 baada ya kuhitimu masomo
(d) TZS 139,500.00 ni fedha iliyobaki na inakatwa kupunguza deni la mnufaika lililopo HESLB

Utaratibu wa kikokotoo kwa mnufaika asiye na adhabu;

  1. Mnufaika aliyeajiriwa anapaswa kukatwa 15% tu ya mshahara wake

2. Ikiwa mshahara wake ni TZS 1,000,000.00 na ameanza kurejesha kwa wakati atakatwa TZS 150,000.00 (15%) tu

3. Makato ya TZS 150,000.00 yatagawanywa kama ifuatavyo:
(a) TZS 1,500.00 ambayo ni Tozo ya 1% ya Uendeshaji (Loan Administration Fee – LAF)
(b) TZS 9,000.00 ambayo ni Tozo ya 6% ya kutunza thamani ya fedha za mkopo uliopewa ukiwa masomoni. (Hata hivyo Rais Samia Suluhu Hassa alielekeza HESLB kuondoa tozo hii)
(c) TZS 139,500.00 ni fedha iliyobaki na inakatwa kupunguza deni la mnufaika lililopo HESLB

Chanzo: HESLB

Send this to a friend