Kauli ya Malecela kuhusu Machifu na utendaji wa serikali

0
24

Siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kusimikwa kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania, kisha kupewa jina la Chifu Hangaya, lenye maana ya nyota inayong’aa, kumeibuka mijadala mingi hasa kuhusu kiongozi wa serikali kuwa chifu, huku wengine wakidai vyeo cya uchifu vilikwisha kufutwa.

Haya hivyo, Makamu wa Rais Mstaafu, John Malecela amesema kuwa serikali haikatazi uwepo wa machifu bali ilitunga sheria ili kutengenisha utendaji wa kichifu na wa kiserikali, na sio kufuta uongozi huo wa kimila.

“Na hata sasa serikali inasisitiza machifu watusaidie kudumisha mila na tamaduni zetu na pale ambapo nyingi zimepitwa na wakati, tuzione na tuziseme kwa wazi,” amesema Malecela akinukuliwa na gazeti la Mwananchi.

Serikali ilipitisha sheria bungeni mwaka 1961 kutenganisha utendaji wa machifu na utendaji wa serikali.

Send this to a friend