Dalili 6 za ukosefu wa nguvu za kiume

0
19

Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi kwa wakati linaweza kuathiri maisha ya mhusika kwa kiasi kikubwa sana.

Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:

1. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara. Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote.

Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayoi ndio inayo hufanya uume usimame barabara.

2. Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa mara moja. Hii husababishwa na kutokuwa na msukumo mzuri wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume.

3. Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa. Hili ni matokeo ya kuwa na msongo wa mawazo.

4. Kufika kileleni mapema.

5. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa. Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume linapokuwa limekomaa.

6. Uume kusinyaa na kurudi ndani. Hapa uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa hali hii husababishwa na upigaji punyeto kwa mda mrefu pia magonjwa hasa chango la kiume au ngiri.

Vyanzo vikuu vya ukosefu wa nguvu za kiume ni:

  1. Upigaji punyeto wa mda mrefu
  2. Msongo wa mawazo
  3. Ugonjwa wa kisukari
  4. Shinikizo la damu (pressure)
  5. Kupooza kwa mwili
  6. Kuugua chango la kiume
  7. Ulevi ulokithiri
  8. Woga wa kufanya tendo la ndoa
  9. Kuwa na wasiwasi wa kumudu kutekeleza tendo la ndoa
  10. Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za nyuma
  11. Ulaji mbovu wa vyakula vya kisasa na vyenye mafuta kupita kiasi
  12. Mazingira yasiyoridhisha wakati wa tendo la ndoa

Makala hii imeandikwa na Nicolaus Mwamposa (@nicomwamposa)

Send this to a friend