Akauti 25 za ku-follow Twitter Tanzania (Oktoba – Disemba 2021)

0
34

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania imeongezeka kutoka milioni 26.8 Julai mwaka 2020 mpaka 29.1 Aprili 2021, sawa ongezeko la asilimia 8.3.

Kwa mujibu wa ripoti ya Digital 2021, iliyotoka Februari mwaka huu zaidi ya Watanzania milioni 5 wanatumia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kila siku, watu wanajiunga kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii, na wakati mwingine hupata changamato kuanza hasa pale wanapokuwa hawana wafuasi. Kuna watu wengi sana kwenye mtandao wa Twitter ambao huchapisha maudhui mbalimbali, kati ya hao wengi, tumekuandalia orodha ya akaunti 25 za kufuata, ambazo zinawakilisha maelfu ya nyingine zilizopo.

Mpangilio huo haujafuata umuhimu wa akaunti husika, na uchaguzi huu unawakilisha akaunti nyingine nyingi ambazo isingewezekana kuziorodhesha zote.

1.Gillsants (@GillsaInt)

Kwa vile tu hakuna barua ya udahili, ukurasa huu ulipaswa kuwa chuo cha kati. Kubwa utakalopata kwake ni elimu ya ujasiriamali kwa kutumia mitandao ya kijamii. Atakupa mbinu za kutumia kugeuza simu yako kuwa ofisi na kujiingizia kipato. Sema kuna wakati anafanya wenye kipato kidogo wajione kama mapenzi si fani yao 😂.

2. Martin M. M (@IAMartin_)

Katika ngazi za mahakama, pengibe itafutwe namna ya kuingiza ukurasa huu nao uwe mahakama. Kupitia ukurasa huu utajua yote yanayojiri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

3. Madenge (@rollymsouth)

Tuseme tu huyu ni kiraka, tuishie hapo, maana ni afisa wa benki, influencer, mwigizaji, kocha wa uhusiano. Kwenye ukurasa wake utapata habari mchanganyiko.

4. Tunzaa (@tunzaaHQ)

Hapa utaweza kununua bidhaa bora na zikaletwa popote ulipo. Haya ni mapinduzi ya ufanyaji biashara Tanzania, ukiwa ni ubunifu wa kijana wa Kitanzania

5. Masoud Kipanya (@masoudkipanya)

Baadhi ya watu waamini ni muda mwafaka sasa atunukiwe PhD. Moja kati ya wachora katuni mahiri Afrika, katuni zitakazoukimbiza ubongo wako kujaribu kuzielewa.

Njia 6 za kutambua akaunti feki (parody) Twitter

6. Togolani Mavura (@tonytogolani)

Maarifa ya namna ya kuenenda katika maisha utayapata hapa bure kabisa. Ila nadhani ni wakati sasa watu wamjue Mshauri wa Masuala ya Kipumbafu, wakati mwingine anachomesha utambi.

7. dɛmɪɡɒd (@Blizzss)

Unataka kujua wapi kuna biriani tamu, au chips za wapi tamu zaidi Dar. Kiufupi kama we ni mtu wa misosi, pita hapa, hutojuta. Lakini pia masuala ya movies, electronics, na vimaswali vya ajabu yamesheheni.

8. UDADISI (@Udadisi)

Ukurasa huu ni chuo kikuu, utapata uchambuzi wa kina wa matukio yanayotokea nchini, hasa ya kisiasa. Kupitia blogu yake, Udadisi huchapisha machapisho ya wanazuoni mbalimbali, ambayo ni muhimu kuyasoma kuweza kulitazama jambo kwa upande wa pili. Sifa nyingine ni matumizi ya kiswahili, huenda ukahitaji kamusi ya Kiswahili ukipitia ukurasa wake.

9. TOTRunners (@TOTRunners)

Jina linasadifu maudhui. Kama wewe ni mwanamazoezi (hasa kukimbia), fika hapa. Lugha zao ni pace, pacer, km, mama mkanye mwanao, medal, water points, challenges. Unaweza usiwaelewe kama sio mwanafamilia.

10. Digital Migrant (@DigitalMigrant1)

Hapa ni ufala tu, hakuna cha maana.

Twitter yazindua huduma ya kutuma ujumbe kwa sauti

11. MichaelMwebe (@MichaelMwebe)

Habari na uchambuzi na taarifa za soka za ndani na nje ya nchi, unapatikana hapa, hakuna mengi wala mbwembwe.

12. Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai)

Kwake utapata zaidi mijadala kuhusu haki za binadamu, demokrasia na vya kufanana navyo.

13. Kuduishe Kisowile (@Kudu_ze_Kudu)

Daktari mwandishi atakupatia hints mbalimbali kuhusu afya yako na masuala mbalimbali ya kijamii. Mara moja moja utona tweets za kulalamikia daladala na tupicha picha akienda dates.

14. Tanzania Business Insight (@TanzaniaInsight)

Huu ni kwa wale ambo wana Kiingereza cha kuchezea, kama chako ni kwa ajili ya interviews tu, kaa mbali. Habari mbalimbali kwa lugha ya Kiingereza.

15. SwahiliTimes (@swahilitimes)

Si mnaona tunavyowakalisha. Tufuate kwa habari bila mipaka saa 24, na mengine ya kibunifu kama hivi.

Mbinu ya wadukuzi (hackers) katika kudukua akaunti yako Twitter, Instagram au Facebook

16. Samia Suluhu (@SuluhuSamia)

Yani unataka ushawishiwe kumfuatilia Rais wa nchi yako? Tusifike huko.

17. Ruvu Shooting Football Club (@Ruvu_shootingFc)

Wazee wa mipapaso wanalichangamsha sana soka la bongo mitandaoni. Namna yao ya kuandika tweets kwa njia ya ucheshi inapendwa na wengi, hadi vilabu vingine vimeanza kufanya hivyo.

18. Jabir,J.A (@bajabiri)

Mwalimu, mjasiriamali, influencer anayeijua kazi yake, tuseme pia ni mchekeshaji.

19. Msemaji Mkuu wa Serikali (@TZMsemajiMkuu)

Taarifa zote za serikali zinapatikana hapa, fuatilia uweze kujua mipango ya serikali ya nchi yako.

20. ‘THE’ Adam (@Adambrv)

Zile Life Hacks utazipata hapa. Anakuletea taarifa za nyumba bora iweje, hujakaa vizuri anakupa wazo la biashara na kama unayo tayari, basi atapata wazo la namna ya kuiboresha. Yeye anamwaga mchele, anawaachia kuku wale wawezavyo.

Mbinu 24 za kuwa mtu mwenye ushawishi (influencer) katika mtandao wa Twitter

21. Masanja (@mkandamizaji)

Mjasiriamali, mchungaji, mtangazaji, mchekeshaji na mbishi wa Twitter. Unaweza kukuta anabishana na kundi la watu. Lakini utapata jumbe za kukutia moyo, neno la Mungu, mawazo ya kijasirimali.

22. ElimikaWikiendi (@ElimikaWikiendi)

Kila wikiendi tunakusanyika kwenye jamvi hili linalolenga kukuza lugha ya Kiswahili kujadili masuala yatakayotuelimisha. Kupitia watoaji mada utaweza kujua mambo mbalimbali ya kiafya, historia, siasa, uchumi n.k.

23. Book Mart (@BookMarttz)

Kwa wale book worms, basi shida uhitaji wenu unaishia hapa. Utapata vitabu vya kila namna, chagua wewe tu ni chakula gani unataka kuulisha ubongo wako.

24. OsseGrecaSinare (@OsseGrecaSinare)

Kama unataka kuitalii Tanzania ukiwa sebuleni, basi imeisha hiyo. Anayajua machimbo ya utalii, anajua kupiga picha anajua kuandaa makala. Hutochoka kuperuzi picha na kutazama mandhari ya kuvutia ya Tanzania.

25. Millardayo (@millardayo)

Hapa utaweza kufahamu habari mbalimbali zinazojiri ndani na nje ya nchi, exclusive za wasanii na masuala mengine yahusuyo habari.

Hapa chini naweka 3 Honorable Mentions:

1.Fatma Karume – Shangazi (@fatma_karume)

Anasaidia dictionary zetu zisipate vumbi maana anatupa kazi sana sometimes na vibomba.

2. Kigogo (@kigogo2014)

Siku hizi wamemvuruga sana Twitani ila Kigogo ni kigogo, huwezi kujua. Keep refreshing

3. Carol Ndosi (@CarolNdosi)

Scholarships, ujasiriamali, usalama mtandaoni, mambo mengi ya kujenga. ukiona sentensi imeanza na maneno, ‘Don’t Send…’ ujue ni yeye.

Send this to a friend