Tanzania kutoa takwimu za Corona kila wiki

0
21

Serikali imesema kuwa inatakuwa inatoa takimu za maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Korona (UVIKO19) kila wiki, huku ikiwahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa kutoa takwimu hizo ni kuuthibitishia umma kwa ugonjwa huo bado upo kama ambavyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linavyotaka.

Waziri Gwajima aagiza madaktari wanaopotosha kuhusu Corona wawajibishwe

Ameongeza kuwa takwimu hizo zitapatikana mtandaoni na kwenye tovuti ya WHO badala ya kutolewa kwenye mkutano na vyombo vya habari kwani haitowezekana kuifanya mikutano hiyo kila siku.

Tangu Juni mwaka huu Tanzania ilikuwa ikishinikizwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kutoa takwimu za ugonjwa huo nchini ikiwa ni sharti la kupata mkopo wa dharura wa $574 milioni.

Rais Samia alivyombana Askofu Gwajima hadharani chanjo ya Corona

Hadi Oktoba 2, 2021 jumla ya watu 595,938 walikuwa wamepata chanjo ya UVIKO19 nchini Tanzania, na serikali inatarajia kupokea chanjo nyingine za Sinopharm kutoka China mapema mwezi huu.

Mambo ya kufahamu kuhusu chanjo ya Sinopharm inayoletwa nchini kutoka China

Send this to a friend