Rais Dkt. Mwinyi aeleza sababu ya ndege kupokelewa Zanzibar

0
20

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa leo imekuwa siku ya historia kufuatia tukio la ndege mbili mpya za serikali kupokelewa visiwani humo, ikiwa ni mara ya kwanza.

Dkt. Mwinyi amesema hayo akihutumia mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali waliofika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kupokea ndege hizo mbili aina ya Airbus 220-300, ambazo zimefanya ndege zilizonunuliwa kufikia 11.

“Bila ya shaka uamuzi wa kufanya mapokezi haya Zanzibar ni kielelezo cha juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na viongozi wa Taifa hili katika kuendeleza na kulinda fikra, mawazo na falsafa za waasisi wa Taifa letu katika kuulinda na kuudumisha muungano wetu,” amesema Dkt. Mwinyi.

Kati ya ndege tisa zilizokuwa zimewasili nchini kabla ya leo, nane zilipokelewa jijini Dar es Salaam huku moja (Boeing 787 – 800 Dreamliner) ikipokelewa jijini Mwanza.

Dkt. Mwinyi ameitaka Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kutumia changamoto za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19) kama fursa ya kibiashara ili kuweza kuingiza mapato zaidi na wananchi waweze kunufaika na ndege hizo.

Pamoja na mambo mengine, ndege zilizopokelewa leo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 132 (12 daraja la biashara na 120 daraja la uchumi), zinaweza kuruka kwa saa sita angani na zina mifumo ya kiusalama na burudani kuhakikisha abiria na marubani wanakuwa salama na kufurahia safari.

Send this to a friend