Rais Samia aitaka UWT kutafiti hali ya kiuchumi ya wanawake tangu uhuru

0
12

Katika kutathmini mchango wa mwasisi wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Bibi Titi Mohamed, Rais Samia Suluhu Hassan ameutak umoja huo kuangalia namna safari yao ilivyokuwa kwa kutazama hali ya kiuchumi, kisiasa na kifikra pamoja na walivyoweza kumkomboa mwanamke.

Raia Samia amesema hayo leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kumbukumbu ya Bibi Titi Mohamed, katika sherehe zilizofanyika kwenye kijiji cha Mkongo Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Amesema ipo haja kwa viongozi wa UWT kujitathimini katika kipindi cha miaka 60 tangu nchi ipate uhuru kuangalia kama wanaendeleza yale yaliofanywa na waasisi wa Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na Bibi Titi Mohamed.

Rais Samia amesema Serikali inatambua mchango wa Bibi Titi alioutoa kwa taifa ambao ulisababisha  Serikali kuipa jina lake katika moja ya barabara ya Jiji la Dar es Salaam kama ishara ya kumuenzi na kutambua mchango wake.

Amewataka watafiti na waandishi katika fani za historia kuandika vyema historia ya Bibi Titi Mohamed ili kuwezesha vizazi vya sasa na vijavyo kujua kikamilifu mchango wake kwa taifa.

Send this to a friend