Rais Samia kufanya ziara ya siku 3 nchini Misri

0
13

Rais Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Misri kuanzia kesho Novemba 10, 2021 kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah Al Sisi.

Katika ziara hiyo, Rais Samia pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.

Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja na hati saba za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.

Send this to a friend