Majina ya Wachungaji 7 wa KKKT waliovuliwa/kusimamishwa Uchungaji

0
26

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (DKMs) limewachukulia hatua mbalimbali viongozi nane kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kusimamia mali za Dayosisi katika uongozi wao.

Sababu nyingine zilizopelekea viongozi hao kusimamishwa ua kuvuliwa uchungaji ni kutumia vibaya madaraka yao kulikosababisha uvunjwaji wa katiba ya kanisa.

Aidha, viongozi hao wamedaiwa kufanya mambo yanayosababisha migongano na hivyo kuchochea vurugu na ukosefu wa amani miongoni mwa waumini na watumishi wa dayosisi kwa ujumla.

Waliochukuliwa hatua mbalimbali ni:
1. Dkt. Stephen Ismail Munga, aliyekuwa Askofu wa Dayosisi na Mdhamini wa mali amevuliwa uchungaji na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Askofu Mstaafu wa DKMs

2. Mchungaji Dkt. Ebert Hardt Ngugi, aliyekuwa Msaidizi wa Askofu na Madhamini wa mali. amesimamishwa uchungaji

3. Mchungaji James Mwinuka, aliyekuwa Katibu Mkuu na Mdhamini wa mali amesimamishwa uchungaji

4. Mchungaji Dkt. Anneth Munga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo-SEKOMU, amesimamishwa uchungaji

5. Mchungaji Yambazi Mauya, Aliyekuwa Mkuu wa Jimbo (Dinari) la Tambarare amesimamishwa uchungaji

6. Mchungaji Paulo Diu, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Kikristo na Elimu amesimamishwa uchungaji

7. Mchungaji Yona Titu, aliyekuwa Chaplain wa Hospitali ya Bombo, amesimamishwa uchungaji

8. Rodgers Shehumu, aliyekuwa Mtunza Hazina wa Jimbo la Tambarare na Hospitali ya Lutindi, amesimamishwa kazi.

Katibu Mkuu wa DKMs, Mchungaji Godfrey Walalaze amewasihi waumini kuwa watulivu na kuendelea kuombea amani ya kanisani na dayosisi kwa ujumla.

Send this to a friend