Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amethibitisha kushiriki kwa njia ya mtandao Mkutano wa Viongozi Wanaume ulioitishwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felex Tshisekedi utakaofanyika Novemba 25, 2021.
Ametoa ahadi hiyo leo akishiriki Mkutano wa Viongozi Wanawake Barani Afrika (AWLN) uliofanyika kwa njia ya mtandao, kujadili masuala ya kuwainua wanawake kiuchumi katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Rais Samia amewafahamisha washiriki wa mkutano huo kuwa tayari ameanzisha mabaraza ya kuwawezesha Wanawake kiuchumi katika ngazi mbalimbali nchini Tanzania ikiwa ni moja ya nguzo za mtandao huo.
Ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kutengeneza Sera na Mifumo ya Kisheria itakayowezesha wanawake kuinuliwa kiuchumi.
Mtandao wa Viongozi Wanawake Barani Afrika (AWLN) unaongozwa na nguzo sita zenye lengo la kuchochea Ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa na ile ya 2063 ya Umoja wa Afrika (AU).