Rais Samia asema Safina ya Nuhu iliishia Tanzania

0
30

Kutokana na idadi kubwa ya wanyama na vivutio vya kitalii vilivyopo nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amesema inaaminika kwamba Safina ya Nuhu baada ya kuzunguka miaka mingi, iliishia Tanzania.

Amesema hayo mara baada ya kuzindua hoteli ya kifahari ya nyota tano, Gran Melia Hotel jijini Arusha ambayo pamoja na kutoa malazi kwa wageni, itakuza utalii na kuboresha mandhari na hadhi ya jiji hilo.

Kwa mujibu wa Biblia, safina hiyo ilibeba viumbe mbalimbali kutokana na gharika, na kwamba ni dhahiri iliishia Tanzania kwa sababu ndio nchi yenye wanyama wengi.

Mwekezaji wa hoteli hiyo ana hoteli sita nchini ambazo zimetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 800, huku wakitarajia kuwekeza zaidi nchini.

Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa Uchumi wa Utalii kwa nchi yetu hivyo inafanya jitihada kuimarisha mazingira ya kibiashara kwa kuendeleza na kuboresha miundombinu ikiwemo barabara, reli, anga na usafiri wa maji ili kuweka mazingira mazuri kwa utalii na kuwezesha uwekezaji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22 idadi ya watalii imeongezeka kwa asilimia 248, ongezeko ambalo limechangiwa na utoaji wa chanjo ya UVIKO19.

Send this to a friend