Mahakama ya kupambana na rushwa nchini Kenya imeagiza akaunti ya benki ya ya mwanafunzi, Felesta Njoroge (21) ifungwe kwa siku 90 ili kuruhusu Wakala wa Urejeshaji Mali (ARA) kufahamu chanzo cha TZS bilioni 2.3 zilizopo kwenye akaunti hiyo.
Wakala huyo inashuku kuwa fedha hizo ni matokeo ya utakatishaji wa fedha na hivo ikaomba akaunti ifungwe.
Kwa upande wake mtuhumiwa wa sakata hilo amesema kwamba alipata fedha kutoka kwa mpenzi wake wa Ubelgiji, Marc De Mesel.
Fedha hizo katika akaunti ya Njoroge ambaye ni mwanafunzi Chuo cha Mafunzo Ufundi cha Nairobi ziliwekwa kupitia miamala minne kati ya Agosti 4 na 6, 2021.
Alipoulizwa kuhusu matumizi ya fedha hizo, mwanafunzi huyo alisema mpenzi wake alimtumia kama zawadi na kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya ardhi na utalii.