Mtanzania amuahidi Rais Samia kujenga kiwanda cha kutengeneza simu janja

0
30

Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing Ltd kuhakikisha anakamilisha azma yake ya kujenga kiwanda cha kuzalisha simu janja (smart phone) hapa nchini.

Rais ametoa msisitizo huo leo mara baada ya kuzindua kiwanda hicho cha kutengeneza nyaya kwa ajili ya mkongo wa Taifa na kuongeza kwamba ujenzi wa kiwanda cha simu pamoja na mambo mengine kitachangia utoaji ajira kwa vijana.

Akizungumzia kiwanda alochozindia leo amesema Serikali ina lengo la kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma za mawasiliano ili kuwawezesha kutumia huduma zitonakazo na TEHAMA katika kukuza uchumi nchini.

Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing Ltd kina uwezo wa kuzalisha kiasi cha kilomita 24,000 za optic fiber kwa mwaka na kinatarajiwa kutoa ajira zipatazo 670 kitakapokamilika katika awamu zote na hivyo kukifanya kuwa kiwanda cha tatu kwa ukubwa barani Afrika na cha kwanza kwa Afrika Mashariki na Kati.

Takwimu za serikali za Juni 2021 zilionesha kuwa watumiaji wa intaeneti Tanzania ni milioni 29, huku idadi ya laini za simu ikifika milioni 53.1.

Send this to a friend