UVIKO19: Marekani yaiweka Tanzania katika orodha ya nchi hatarishi kutembelea

0
24

Marekani imeijumuisha Tanzania katika orodha ya nchi sita ambazo imewatahadhari raia wake kuzitembelea.

Kituo cha kuzuia na kupambana na magonjwa cha Marekani (CDC) kimeiweka Tanzania pamoja na Ufaransa, Jordan, Andorra, Cyprus na Lichtenstein katoka orodha ya nchi ambazo haiwashauri raia wa Marekani kutokana na hatari ya kupata maambukizi ya UVIKO19.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa endapo itamlazimu raia wa Marekani kufika Tanzania basi ahakikishe amechanjwa kabla ya kusafiri.

Licha ya maelekezo ya serikali kuwataka Watanzania kuchukua tahadhari kama kutoshiriki mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono, kuchanjwa, kutumia vitakasa mikono, bado mwitikio ni mdogo sana.

Takwimu zilizotolewa na Tanzania hadi Novemba 28 mwaka huu zinaonesha kuwa jumla ya visa 26,273 vimerekodiwa ambapo vifo ni 731.

Send this to a friend