Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, ametunuku Nishani 14 ikiwa ni sehemu ya Nishani 893 alizozitunuku kwa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini.
Waliotunukiwa Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru ni;
1. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo
2. Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Simon Nyakoro Sirro
3. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Kamishna Diwani Athumani Msuya
4. Mkuu wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee
5. Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali John William Masunga
6. Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Kamishna Jenerali, Dkt. Anna Peter Makakala.
Waliotunukiwa Nishani ya Utumishi Uliotukuka ni;
1. Meja Jenerali Hawa Issa Kodi,
2. Kamishna wa Polisi Shaban Mrai Hiki
3. Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mkwanda Hasseid Mkwanda.
Waliotunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema ni;
1. Afisa Mteule Daraja la I, Martin Peter Kazilo kutoka JWTZ,
2. Mkaguzi wa Polisi, Stahmil Herman Lusatila
3. Mkaguzi wa Magereza, Nicerosiana Elisa Malisa
4. Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Ishima Shomari Seif
5. Mkaguzi wa Idara ya Uhamiaji, Abubakary Muhonzi Yunusu