Mtoto wa miaka 10 milionea anayekusudia kustaafu akiwa na miaka 15

0
32

Licha ya kuwa shule ya msingi, mtoto wa kike kutoka Australia anaelekea kustaafu akiwa milionea akiwa na umri wa miaka 15.

Pixie Curtis mwenye miaka 10 alianzisha kampuni ya midoli ambayo inamuingia kiasi kikubwa cha fedha.

Kwa msaada wa mama yake, Roxy Jacenko, Pixie aliweza kuanzisha kampuni yake, Pixie’s Fidget ambayo aliizindua mwaka uliopita, na kuuza midoli yote ndani ya saa 48.

Mbali na hilo, ana kampuni nyingine, Pixie’s bow, kampuni ya vifaa vya nywele ambayo mama yake aliinzisha wakati akiwa mtoto. Kampuni zote hizi ni sehemu ya Pixie’s Pix, ambayo pia inauza vifaa vya michezo ya watoto.

Mama yake amesema kwamba mwanae anaweza kustaafu akifikisha umri wa miaka 15 endapo atataka kufanya hivyo.

Jacenko ni mmiliki wa biashara mbalimbali ambazo zinafanya vizuri ikiwemo kampuni ya Sweaty Betty PR.

Send this to a friend