Chama cha wasioamini katika Mungu Kenya kinatafuta wanachama baada ya katibu wake kujiuzulu na kuwa Mkristo

0
24

Chama cha wasioamini katika uwepo wa Mungu au miungu mingine kimetangaza kuwa kitagharamia matibabu na mazishi, ikiwa ni njia ya kuvutia wanachama wapya.

Jamii hiyo ya wasioamini nchini Kenya (Atheists In Kenya) kimechukua hatua hiyo baada ya kupata pigo mwaka 2021 kufuatia katibu mkuu wake kujiuzulu na kuwa Mkristo.

Jamii hiyo imemsihi yeyote asiyeamini, anayeamini kwamba hakuna chochote kinachoweza kujulikana kuhusu uwepo au asili ya Mungu, mwenye mitazamo huru au anayetilia shaka mambo yanayoaminiwa, kujiandikisha kama mwanachama kupitia tovuti yao na kulipa ada ili kuweza kupatiwa huduma za kugharamia matibabu na mazishi.

Zaidi ya asilimia 97 ya raia wa Kenya ni wenye imani katika dini, kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Pew.

Send this to a friend