Jeshi Polisi: Askari aliyejiua hastahili heshima ya kuzikwa kijeshi

0
52

Jeshi la Polisi limeeleza kwa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Grayson Mahembe alijinyonga hadi kufa akiwa mahabusu kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria kwa kumnyang’anya fedha na kisha kumuua Musa Hamis.

Taarifa ya polisi ambayo imetolewa ili kufafanua tukio halisi kutokana na uwepo wa uzushi imeeleza zaidi kwamba baada ya kutekekeleza mauaji hayo aliutupa mwili wa kijana huyo kichani katika Kijiji cha Namgogori mkoani Mtwara Januari 5 mwaka huu.

Imeelezwa zaidi kwamba baada ya kufanya tukio hilo akiwa na wenzake hawakutoa taarifa kwa viongozi wao kwa sababu walijua wamefanya hivyo kwa nia ovu, kwa tamaa zao na kinyume na sheria ya nchi.

Baada ya polisi kupata taarifa waliwakamata watuhumiwa akiwemo Mahembe ambaye alihojiwa na kuwapeleka polisi eneo ya la tukio.

Watuhumiwa hao kila mmoja aliwekwa kwenye mahabusu yake mwenye lengo likiwa wasiharibu upelelezi uliokuwa unaendelea endapo wangekaa sehemu moja. Akiwa mahabusu Mahembe alijinyonga na uchunguzi wa eneo la tukio na hospitalini vinathibitisha hilo.

Kuhusu kutokuzikwa kijeshi, taarifa hiyo imeeleza kwamba askari anayefariki kwa kujitoa uhai hazikwi kijeshi, kwa maana kwamba hakuna gwaride la mazishi na risasi au mabomu ya kishindo kwa sababu inahesabiwa kwamba hakufa kishujaa hivyo hastahili heshima hiyo.

Send this to a friend