Mwanafunzi: Ninajisikia vizuri kusomea kwenye madarasa mapya

0
27

Walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari JJ Mungai, pamoja na wazazi katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Iringa wameeleza furaha yao kufuatia ujenzi wa madarasa ndani ya kipindi kifupi tofauti na awamu za nyuma ambapo ingechukua muda mrefu kukamilika kwa mradi huo.

Kelvini Tindi ni mmoja wa wanafunzi ambaye anaelezea siku ya kwanza kufika kwenye madarasa hayo na hali aliyokutana nayo.

“Kwanza siku ya kwanza kuingia katika hili darasa nilijisikia vizuri kwa sababu miundombinu ilivyoboreshwa,” amesema Kelvini.

Mwamsumbi Peter ni mzazi wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, naye ameelezea furaha yake na pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kukamilisha ujenzi wa madarasa ndani ya muda mfupi.

“Viti vimekuwepo, watoto wanafuraha kwa hiyo yamekuwa madarasa ya mfano alafu kinachonishangaza ni kwamba ni muda mfupi kumbe mambo yanawezekana. Ni kipindi cha mwaka mmoja toka yaanze kufanyika haya ndio maana inanishangaza, huu ni usimamizi mzuri wa serikali yetu,” amesema Peter.

Send this to a friend