Fahamu namna ya kukabiliana na hasira

0
56

Hasira ni ono linalowapata binadamu na wanyama pasipo kujizuia. Katika hali hiyo mtu hughadhibika, hata kuchukia kwa kupatwa na kitu ambacho yeye mwenyewe hapendi.

Mtu mwenye hasira ya mara kwa mara, hushauriwa ajaribu kuepuka mambo au vitu vinavyomuudhi, kwa mfano, anaweza kuondoka mahali penye maudhi, na kama ni kubishana aweze kunyamaza ili kuepukana na ugomvi.

Pia inashauriwa kuwa, kama unajua mwenzio hukasirishwa na kitu fulani, bora usimchokoze, kwa sababu ni hatari kwa maisha yako na pia kwa hasira yake anaweza kufanya kitu chochote kibaya.

 

Isiporatibiwa na mhusika inaweza ikasababisha madhara makubwa, kama mithali ya Kiswahili isemavyo, “Hasira, hasara.” Hasira hupelekea mtu kuvunja sheria kwa kujichukulia hatua mkononi na mwishowe kufanya jambo la hatari, hivyo mtu mwenye hasira anashauriwa kutafuta suluhu ya vitu vinavyojirudia ili kuepusha madhara anayoweza kuyafanya

Watafiti kutoka nchini Marekani walibaini kuwa hasira kali inaweza pia kumsababishia mtu akapatwa na mshtuko wa moyo au hata kupatwa na kiharusi na hasa wale wanaotoka katika familia zenye historia hiyo, kwa kuepusha hilo unashauriwa kufanya mazoezi ya kila siku pamoja na kutafakari ili kujitafutia suluhisho.

Send this to a friend