Watoto milioni mbili hatarini kupoteza Maisha

0
29

Mkuu wa Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa (UN), Martin Griffiths amesema Watoto wapatao milioni mbili barani Afrika wapo katika hatari ya kupoteza Maisha kutokana na njaa.
Akizungumza katika mkutano wa wahisani uliofanyika Geneva Nchini Uswiss, ameeleza kuwa Watoto hao wapo katika Nchi za pembe ya Afrika ambazo zinakabiliwa na ukame katika kipindi cha miaka kumi sasa, huku akiitaja Nchi ya Kenya, Ethiopia na Somalia kukabiliwa na ukame takribani miaka 40.
Aidha, Griffiths amesema Shirika lake limepata sehemu tu ya fedha zinazohitajika kukabiliana na ukame, hivyo amewataka wahisani kuchukua hatua za haraka kukabiliana na mgogoro wa Ukraine ambao umeiweka Dunia katika taharuki.
Hata hivyo Mashirika ya wahisani wameahidi kuchangia kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 1.4 ili kukabiliana na janga la njaa.

Send this to a friend