Mamlaka ya Udhibiti Usafiri ardhini (LATRA), leo Aprili 30, 2022 imetagaza viwango vipya vya bei ya nauli za daladala na mabasi ya mikoani itakayoanza kutumika kuanzia Mei 14, mwaka huu.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gillard Ngewe ametangaza viwango hivyo huku nauli ya wanafunzi ikibaki kuwa shilingi 200.
Mkurugenzi ameeleza kuwa kwa mabasi ya mjini kuanzia Kilometa 0 hadi 10, nauli itakuwa TZS 500 badala ya 400 na nauli ya TZS 450 itakuwa ni TZS 550.
Kwa kilomita 30 nauli itakuwa TZS 850 badala ya TZS 750 na kwa kiliometa 35 nauli itakuwa TZS 1000 na kwa upande wa Kilometa 40 nauli itakuwa TZS 1100, amesema Ngewe.
Amesema kwa mabasi ya mkoani daraja la kawaida kwa Kilometa 1 imeongezeka kwa asilimia 11 kutoka TZS 36 kwa kilometa moja hadi TZS 41, na daraja la kati imeongezeka kwa asilimia 6, hivyo abiria mmoja atalipa TZS 56.88 kwa kilometa kutoka TZS 53.