Wanawake waongoza Magonjwa ya Ngono Simiyu

0
31

Kamati ya Ukimwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, imesema kuwa katika Wilaya hiyo takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wanaongoza idadi ya maambukizi ya magonjwa ya ngono zaidi ya wanaume.

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Diwani Christopher Ndamo wakati akiwasilisha taarifa ya kamati yake kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya, akieleza kuwa wanawake 226 wameambukizwa huku wanaume wakiwa 75.

Ameongeza kuwa sababu za wanawake kuongoza maambukizi hayo ni kutokana na uwepo wa biashara ya ngono inayofanyika katika Wilaya hiyo, pamoja na wajawazito kuhudhuria kliniki bila wenza wao hivyo kushindwa kupatiwa elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa hayo.

Aidha amesema kuwa kamati hiyo imewaomba Madiwani kuhamasisha jamii kutumia Kondomu kama kinga muhimu ya magonjwa hayo pamoja na UKIMWI.

Send this to a friend