Tanzania yanyemelea fursa ya kuandaa Tuzo za MTV 2023

2
18

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu ameongoza kikao cha awali kati ya wizara na Wawakilishi wa Waandaaji wa Tuzo za Muziki za MTV (THE MTV Africa Music Awards) kutoka nchini Afrika Kusini kujadili kuhusu Tanzania kuandaa Tuzo hizo Kwa mwaka 2022/23.

Katika kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dodoma, Yakubu ameeleza utayari wa wizara kushirikiana na kampuni hiyo kwa kuwa ni fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania ili kuvutia wawekezaji na watalii wengi duniani kuja nchini.

“Tumeona wasanii wetu watapata nafasi ya kujitangaza na kutangaza Sanaa ya Tanzania duniani, kuna fursa pia ya kutangaza nchi yetu katika utalii hivyo tumepokea wazo na tutalijadili na kutoa mrejesho wenye tija,” amesema Naibu Katibu Mkuu Yakubu.

Kwa upande wa mwakilishi kutoka MTV,  Kabelo Ngakane amesema kufanyika kwa tuzo hizo kutatoa nafasi kwa wasanii mbalimbali ikiwemo wanamuziki, wanenguaji (Dancers), watayarishaji wa muziki, watangazaji kupata elimu pamoja na ujuzi mbalimbali katika kukuza Sanaa zao.

Send this to a friend