Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hamza Hassan Juma ametoa sababu mbalimbali za kufungwa kwa vituo 10 vya polisi ikiwemo changamoto za uendeshaji wake na kuimarika kwa ulinzi shirikishi.
Ameyasema hayo katika Baraza la Wawakillishi Zanzibar alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Machano Othman Said ambaye alitaka kujua sababu za kufungwa kwa vituo hivyo wakati wananchi wanahitaji kulindwa na mali zao.
Waziri amebainiisha kuwa vituo hivyo vilivyofungwa kwa nyakati tofauti tofauti vilichangiwa na gharama za uendeshaji zilizopelekea uhaba wa askari.
Aidha, amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza na kusimamia majukumu yake kwa mujibu wa sheria ikiwemo ulinzi wa raia na mali zao.
Alifafanua zaidi kwamba Jeshi la Polisi halitasita kufungua vituo vipya ili kukabiliana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea nchini.