Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema wabunge 19 wa Viti Maalum, pamoja na kukata rufaa haikuwa tiketi ya wao kuendelea kubaki bungeni huku wakiwa wamefukuzwa uanachama.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es samaam, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Benson Kigaila amesema ili mtu aendelee kuwa mbunge ni lazima awe na udhamini wa chama cha siasa, hivyo walitakiwa kuondolewa ubunge pindi walipovuliwa uanachama.
Aidha, Kigaila amesema wabunge hao wamekuwa wakitoa malalamiko ya kutokusikilizwa ilihali walipewa nafasi ya kusikilizwa mara kadhaa lakini hawakuweza kusema chochote.
“Unamsikilizaje mtu ambaye kikao cha kwanza cha kamati kuu ulimuita aje hakuja? Kikao cha pili cha rufaa pamoja na kwamba rufaa sio kikao cha kusikiliza shauri lakini umempa nafasi ya kusema chochote anachotaka kusema hakusema, lakini akitoka nje anasema hakusikilizwa, kusikilizwa kuna maana gani?” amesema
Mdee na wenzake wakata rufaa mahakamani, bunge lashindwa kutoa mamuzi
Ameendelea kueleza ili mtu aapishwe kuwa mbunge lazima mambo mawili yakamilike, kamati kuu lazima ifanye uteuzi kuthibitisha uteuzi huo, lazima katibu mkuu wa chama (John Mnyika) aiandikie barua tume kuwa CHADEMA imeteua orodha hiyo.
Hivyo, fomu ambazo tume hupeleka kwenye vyama ili wateuliwa wajaze ziko kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na hazijajazwa na mtu yoyote.