Daktari aeleza sababu za wanaume kufa zaidi kwa UKIMWI

0
23

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko amesema ripoti mpya inaonesha kwamba wanaume wanaongoza kwa vifo vitokanavyo na Virusi vya Ukimwi huku wanawake wakiongoza kwa maambukizi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa wahariri na waandishi wa habari, Dk. Maboko amesema kwamba wanaume wako nyuma kujitokeza kupima na wako nyuma kutumia ARVs (dawa za kupunguza makali ya VVU).

“Wanawake ni wepesi kupima na wanatumia vizuri dawa. Tunamshukuru Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekubali kuwa balozi wa wanaume kuhamasisha upimaji kujua hali ya maambuki ya VVU,” amesema.

Aidha, kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2021, watu 54,000 nchini wamepata maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU), idadi ambayo imepungua kulinganishwa na mwaka 2020 ambapo watu 68,000 walipata maambukizi mapya.

Dk. Maboko amesema makadirio mapya yanaonesha vijana wanaendelea kuwa kundi lililo hatarini zaidi dhidi ya UKIMWI, hivyo programu nyingi sasa zimeelekezwa kwa kundi hilo.

Send this to a friend