Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa kusimima nidhamu ya wauguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo kuzuia kutumia lugha isiyo rafiki kwa wagonjwa.
Amesema hayo leo jijini Dodoma katika kikao cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe nchini kilichowahusisha waganga wakuu wa mikoa, maafisa lishe wa mkoa na wadau wa lishe.
“Kwenye ziara zangu nimekuwa nikikumbana na kero za wananchi wakati wakipatiwa huduma ikiwemo kauli zisizo rafiki kwa baadhi ya Wauguzi kwa wagonjwa, na nitumie nafasi hii kuwaelekeza waganga wakuu wa mikoa kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi katika vituo vyetu vya kutolea huduma,” amesema Bashungwa
Msisikilize maneno ya watu wa pembeni, Waziri Mkuu awaambia wakazi wa Ngorongoro
Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea kufanya jitihada kubwa kuhakikisha vituo vya afya, zahanati zinazojengwa na kukarabatiwa pamoja na hospitali za wilaya zinakamilika.