Watatu wafukuzwa kazi kwa kuchelewesha kivuko Kigamboni

0
15

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umewafukuza kazi watumishi watatu wa kivuko cha Magogoni-Kigamboni, Dar es Salaam kwa kuchelewesha kivuko kwa makusudi.

Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa TEMESA imewataja watumishi hao waliofukuzwa kuwa ni nahodha, fundi wa kivuko pamoja na baharia.

CHADEMA: Uandaaji wa kanuni za mikutano ya hadhara ni uhuni

Kwa mujibu wa tarifa kwa umma Mei 24 mwaka huu watumishi hao walichelewesha kwa makusudi kivuko upande wa Kigamboni na kusababisha usumbufu na taharuki kwa abiria wanaotumia kivuko hicho.

Send this to a friend