Madhara ya kiafya ya kuchangia ‘helmet’
Usafiri wa pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ umeshamiri sana nchini Tanzania kwa sababu ni usafiri wa haraka na rahisi. Abiria wanaotumia bodaboda hulazimika kuvaa kofia ngumu (helmet) kwa ajili ya usalama wao.
Kofia hizi mara nyingi hutumiwa pasipo kubadilishwa, hivyo kuhatarisha usalama wa kiafya katika kupata maambukizi ya magonjwa ya ngozi.
Hawa ni abria pamoja na madereva wa ‘bodaboda’ wakieleza ufahamu walionao juu ya athari zinazoweza kujitokeza pindi abiria wanapochangia kofia za usalama.