Waziri Ummy: Marufuku shisha, ugoro

0
46

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) kufanya tathmini ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo Shisha, Ugoro na Sigara za kielektroniki ili kuona namna ya kupunguza au kusitisha kabisa matumizi ya bidhaa hizo ili kulinda afya ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari, waziri amesema sheria ya udhibiti wa bidhaa za Tumbaku imezuia matumizi ya baadhi za Tumbaku kama vile Shisha, Ugoro na Sigara za Kielektroniki zinazotumiwa hususani katika hoteli kubwa zilizoko jijini Dar es Salaam.

“Sheria haijafutwa, bado sheria inasema ni marufuku kutumia shisha, ugoro na sigara za kielektroniki, lakini nafahamu na nyie mnafahamu kwamba bidhaa hizi zimekuwa zikitumika kwa miaka mingi hususani kwa vijana na wazee. Nilichowaambia na kuwaelekeza ni kufanya tathmini ya bidhaa hizi ili kuona namna ya kupunguza au kusitisha kabisa,” amesema.

Aidha, amesema kwa mtu yeyote anayefanya biashara ya shisha ajue kwamba anavunja sheria ya nchi.

Waziri amebainisha utafiti uliofanywa unaonesha bidhaa hiyo ya shisha inachanganywa na bidhaa nyingine ambayo ni sehemu ya madawa ya kulevya.

Send this to a friend