NEMC kufunga makanisa yanayopiga kelele

0
27

Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetangaza kua litazifungia leseni za makanisa na baa zitakaokaidi agizo la kutokupiga kelele katika maeneo ya makazi.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema kelele hizo zinazosababishwa na kumbi za starehe pamoja na makanisa zinaleta adha kwa watu na madhara makubwa ya kisaikolojia pamoja na afya zao, hivyo hawatavumilia tena suala hilo.

“Tutakachofanya sasa ni kuchukua katazo la mahakama na likishapatikana ni kuzifungia kabisa shughuli hizi kwa sababu zinaleta adha kubwa kwa wengi kuliko wanaofaidika nazo,” amesema Gwamaka.

Hata hivyo, ameongeza kuwa upo muda maalum wa kupaza sauti, pia zipo sehemu mahsusi zinazoruhusiwa kuanzisha shughuli za ibada au kujenga kumbi za starehe kwa wanaozihitaji.

Send this to a friend