Wakili: Sabaya ana uvimbe kichwani

0
27

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabilia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne hadi Juni 20 mwaka huu.

Wakiwa mahakamani hapo leo, mawakili wa utetezi wameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo ili Sabaya apelekwe hospitali kutibiwa kutokana na kuwa na uvimbe kichwani.

Wakili Hellen Mahuna amemwambia Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha kuwa mshtakiwa namba moja ambaye ni Sabaya ni mgonjwa na anatakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji.

Amedai mshtakiwa huyo alipata uvimbe huo akiwa kazini, hivyo mawakili wanaomba kesi hiyo iahirishwe ili akafanyiwe upasuaji.

Mbali na Sabaya, wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Odemba Aweyo,Nathan Msuya na Antheo Boniface Assey ambao wanashtakiwa na makosa saba ya uhujumu uchumi ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kutenda kinyume na mamlaka yake, kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.

Send this to a friend